Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugonjwa usiojulikana waua watoto watano nchini Uganda

Malaria Ni Ugonjwa Ugonjwa usiojulikana waua watoto watano nchini Uganda

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto watano wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa usiojulikana nchini Uganda. Ungjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Januari katika vijiji sita vya Wilaya ya Bukomansimbi katikati mwa nchi hiyo.

Baadhi ya wazazi waliopoteza watoto wao wameviambia vyombo vya habari kwamba ingawa walikimbilia hospitalini mara tu watoto wao walipohisi vibaya, madaktari hawakuweza kuokoa wagonjwa wao kwa vile walikuwa wamechelewa.

Viongozi katika eneo hilo wameitaka wizara ya afya ya nchi hiyo kuchunguza kile "kinachowaua watoto wao" huku wakilalamikia uzembe wa maafisa wa afya wa eneo hilo.

Ugonjwa huo wa ajabu una dalili za homa kali, kutapika, kupauka, kutoa mkojo wenye damu, na udhaifu wa jumla wa mwili.

Daktari Alfred Kato, afisa wa afya wa wilaya hiyo, amedai kwamba kuna uwezekano ulikuwa wa malaria kali.

Malaria ni ugonjwa unaoweza kuua ambao unaenezwa na aina maalumu ya mbu, ambao hupatikana hasa katika maeneo ya tropiki. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), bara la Afrika limeathiriwa zaidi na ugonjwa huo, huku asilimia 95 ya visa na asilimia 96 ya vifo vikitokea barani humo,

Aidha, idadi ya wagonjwa wa malaria iliongezeka kwa takriban milioni 5 mwaka 2022 ikilinganishwa na 2021. Kila dakika, mtoto wa chini ya umri wa miaka mitano hufariki dunia kutokana na malaria, kulingana na WHO.

Mojawapo ya njia bora zaidi za kukabiliana na ugonjwa huo ni chanjo. Mnamo Januari, dozi za kwanza za chanjo ya malaria ziliwasilishwa kwa Benin, taifa la tatu la Afrika kupokea chanjo hiyo baada ya Sierra Leone na Cameroon, baada ya awamu ya majaribio nchini Ghana, Kenya na Malawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live