Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugomvi wa wawili wasababisha maujai ya watu 100 mgodini

Mauaji Mgodini Ugomvi wa wawili wasababisha maujai ya watu 100 mgodini

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wasiopungua 100 wameuawa nchini Chad katika mapigano yaliyotokea kati ya wachimba migodi ya dhahabu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Waziri wa Ulinzi wa Chad Jenerali Daoud Yaya Brahim, mapigano hayo yalizuka Mei 23 katika eneo la Kouri Bougoudi karibu na mpaka wa Libya na yalichochewa na ugomvi kati ya wachimba migodi wawili na hatimaye kuripua machafuko makubwa yaliyopelekea watu wengine 40 pia kujeruhiwa.

Jenerali Yaya Brahim ameongeza kuwa, mapigano hayo yalihusisha wachimba migodi raia wa Mauritania na Libya.

Aidha amesema, eneo hilo yalikozuka mapigano hayo la Sahara ya Kati katika milima ya Tibesti liko umbali wa kilomita elfu moja kutoka mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

Akizungumza kwa njia ya simu na vyombo vya habari kutokea mahali yalipozuka mapigano hayo, waziri wa Ulinzi wa Chad amesema, hali ni tete na ya kutia wasiwasi katika eneo la Kouri tangu yalipogunduliwa madini ya dhahabu ambayo yamevutia wachimba migodi wengi kutoka Chad na nchi jirani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live