Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yatinga uchumi wa kati

Museveni Jn.jpeg Yoweri Museveni, Rais wa Uganda

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Uganda imetangaza rasmi kuingia uchumi wa kati mara baada ya kuvuka mdororo wa uchumi uliodumu kwa takribani miaka mitatu nchini humo.

Akizungumzia ongezeko hilo Rais Yoweri Museveni alisema kuwa taifa hilo limeweza kupiga hatua hiyo katikati ya majanga makubwa yanayoendela kupasua ngoma duniani kote.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisi ya Rais imeonesha kuwa uchumi wa taifa hilo kwa sasa ni dola za kimarekani bilioni 45. kwa njia ya ubadilishaji fedha na dola bilioni 131 kwa mfumo wa manunuzi kwa juma moja.

Museveni alifafanua zaidi ongezeko hilo kuwa;

"Hii ina maana kwamba Pato la Taifa kwa kila mtu ni $1046, sasa tumepitisha idadi hiyo ya watu wa kipato cha kati (dola 1,030)”

"Kinachotakiwa sasa ni kuhakikisha kuwa hatushuki katika kiwango mfululizo ndani ya miaka miwili hadi mitatu ili kutangazwa rasmi kuwa nchi ya uchumi wa kati" aliongeza Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live