Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yasitisha marufuku ya uuzaji wa nyama

Uganda Yasitisha Marufuku Ya Uuzaji Wa Nyama Huku Kukiwa Na Mlipuko Wa Magonjwa Uganda yasitisha marufuku ya uuzaji wa nyama huku kukiwa na mlipuko wa magonjwa

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Uganda zimeripotiwa kusitisha marufuku ya hivi majuzi ya uuzaji wa nyama katika mji mkuu, Kampala, huku kukiwa na mlipuko wa ugonjwa kimeta.

Maafisa wa afya wiki iliyopita walikuwa wameweka marufuku na kuamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuchinja ili kupunguza kuenea kwa mlipuko huo.

Lakini Waziri wa Masuala ya Jiji la Kampala Minsa Kabanda siku ya Jumapili aliliambia gazeti la Daily Monitor kwamba marufuku hiyo imesitishwa huku serikali ikiendelea kutathmini athari za ugonjwa huo katika mji mkuu.

Bi Kabanda hata hivyo aliwataka watu kuhakikisha kuwa wanyama wamepimwa kabla ya kuchinjwa.

Wafanyabiashara walikuwa wamepinga marufuku hiyo na kuishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti ugonjwa huo.

Ugonjwa wa kimeta umeripotiwa katika wilaya 40 kote nchini Uganda, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Chanzo: Bbc