Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yaondoa hofu ya kuzuka kwa ugonjwa wa Covid

Uganda Yaondoa Hofu Ya Kuzuka Kwa Ugonjwa Wa Covid Uganda yaondoa hofu ya kuzuka kwa ugonjwa wa Covid

Tue, 9 May 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka ya afya nchini Uganda imeondoa hofu kwamba virusi vya corona huenda ndio chanzo cha wimbi la kikohozi na mafua, ambayo yanashuhudiwa kote nchini.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuongezeka kwa visa vya watu kulazwa kwa siku kadhaa au kupoteza sauti zao kutokana na kikohozi kikali, mafua na homa.

Katika baadhi ya visa, watoto hawajapata ahueni licha ya kutumia dawa na wengine wao wakilazimika kulazwa hospitalini na kuwekwa kwenye mashine za oksijeni, gazeti la Daily Monitor liliripoti.

Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza ilisema mlipuko huo ulikuwa "homa ya kawaida".

"Kwa mujibu wa kwa mfumo wetu wa uchunguzi, hakuna dalili za kuongezeka kwa virusi vya Covid-19," Dk Patrick Tusiime, kamishna wa kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza alisema.#

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba Covid-19 sio tisho tena dharura ya afya ya kimataifa kwa sababu ya kupungua kwa jumla ya watu walioambukizwa.

WHO, hata hivyo, ilionya kwamba watu wengi walio na ugonjwa mbaya wa Covid-19 bado wamelazwa hospitalini na kwamba, nchi zinapaswa kuendelea na hatua za ndani za kukabiliana na ugonjwa huo.

Chanzo: Bbc