Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yalaani pingamizi ya EU kwa mradi wa mafuta

UGANDA WQWE Uganda yalaani pingamizi ya EU kwa mradi wa mafuta

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Uganda limelaani azimio la bunge la Umoja wa Ulaya linalozitaka Uganda na Tanzania kusitisha maendeleo ya miradi yao ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika kikao cha Alhamisi, Naibu Spika wa Uganda Thomas Tayebwa alisema azimio hilo linatokana na taarifa potofu na upotoshaji wa makusudi wa mambo muhimu kuhusu mazingira na ulinzi wa haki za binadamu.

Alisema inawakilisha kiwango cha juu kabisa cha ukoloni mamboleo na ubeberu dhidi ya Uganda na mamlaka ya Tanzania.

Inakuja wakati Uganda na Tanzania zinajenga mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Eacop), lenye urefu wa kilomita 1,443 (maili 896) kutoka Ziwa Albert magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

Pindi litakapokamilika, litakuwa bomba refu zaidi la mafuta yenye joto duniani.

Maoni ya Uganda yalikuja wakati azimio la bunge la Umoja wa Ulaya lililopitishwa siku ya Alhamisi likitahadharisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na hatari ya kijamii na kimazingira inayotokana na mradi wa Eacop.

Bunge la EU linashauri mataifa wanachama kutotoa msaada wowote wa kidiplomasia au kifedha kwa miradi ya mafuta na gesi ya Uganda.

Wanamazingira wamepinga mradi huo kwani unazunguka maeneo yaliyohifadhiwa na mifumo nyeti ya ikolojia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live