Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yakumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta

Uganda Yakumbwa Na Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Kimeta Uganda yakumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Uganda imeweka karantini kwa usafirishaji wa ng'ombe na kupiga marufuku uuzaji wa bidhaa za nyama katika Wilaya ya Kyotera, eneo la kati nchini humo.

Hii inafuatia mlipuko wa ugonjwa wa kimeta ambao hadi sasa umeua watu 17.

Ofisa wa Mifugo wa Wilaya ya Kyotera, John Mary Lutaaya amesema karantini hiyo imewekwa kwa muda huko Kabira, kata ndogo ya wilaya hiyo.

Idara ya mifugo ya wilaya haitoi tena vibali vya kusafirisha ng'ombe kwa wafanyabiashara wa mifugo.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, takriban watu 28 wamelazwa katika vijiji kadhaa vinavyoshukiwa kuwa na ugonjwa wa kimeta, ndani ya Kabira.

Zaidi ya ng'ombe 40 wanaripotiwa kufa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Maafisa wa afya walisema kuwa karantini hiyo itadumishwa hadi madaktari wa afya na mifugo wathibitishe kuwa ugonjwa huo umedhibitiwa.

Kimeta ni ugonjwa nadra lakini mbaya, unaoambukiza unaosababishwa na bakteria (Bacillus anthracis).

Hutokea kiasili kwenye udongo lakini kwa kawaida huathiri wanyama pori na wa nyumbani.

Hata hivyo, watu wanaweza kuambukizwa ikiwa watagusana na wanyama walioambukizwa au bidhaa za wanyama zilizoambukizwa.

Mamlaka ya afya ya Uganda ilithibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa kimeta, Novemba 26. Hapo awali, ugonjwa huo ulikuwa haujulikani wala kutajwa jina tangu watu waanze kuugua huko Kyotera mwezi Oktoba.

Wale walioathirika walipata malengelenge, homa, uvimbe wa miguu na mikono na ugumu wa kupumua.

Baadhi yao wanatembelea maeneo matakatifu badala ya vituo vya huduma za afya na maafisa wa afya wanahofia hii itazuia juhudi zao za kudhibiti mlipuko huo.

Chanzo: Bbc