Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yakashifu Kenya kwa kusambaza COVID-19 kupitia kwa watoto wa shule

D2f3c4b542ca01d3 Uganda yakashifu Kenya kwa kusambaza COVID-19 kupitia kwa watoto wa shule

Fri, 30 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wabunge wa Uganda wamedai kwamba Kenya inasambaza virusi vya COVID-19 kwa nchi yao kupitia kwa watoto wa shule

- Watoto zaidi ya 500 wa shule ya chekechea wamekuwa wakisomea nchini tangu shule zilizpofunguliwa

- Kwa mwaka mmoja Uganda haijafungua shule za chekechea, darasa la kwanza la pili na la tatu

- Mbunge wa munispaa ya Busia Godfrey Macho alisema watoto hao huenda wataambukizwa virusi vya covid-19 na wawaambukize wazazi wao

Wabunge nchini Uganda wameikashifu Kenya kwa kusambaza virusi vya COVID-19 kwa nchi yao kupitia kwa watoto wa shule.

Kulingana na wabunge hao, wanafunzi waliojiunga na shule za humu nchini kufuatia kutofunguliwa kwa shule nchini Uganda, wamekuwa wakibebwa kwenye mabasi kila siku asubuhi na kurejeshwa jioni baada ya masomo.

Wabunge hao walisema kwa sasa zaidi ya wanafunzi 500 kutoka Uganda wanasoma katika shule tofauti na wanahofia kwamba huenda wakaambukizwa virusi vya covid-19 na wavisambaza katika nchi hiyo jirani.

Mbunge wa munispaa ya Busia Godfrey Macho amesema Kenya inazidi kuregodi visa vingi vya maambukizi ya virusi hivyo na ametilia shaka kwamba idadi itaongezeka iwapo tahadhari zinazohitajika hazitafuatwa.

" Shule zinapoendelea kufungwa, kuna wanafunzi kutoka Uganda karibu na mpaka wamekuwa wakienda Kenya kwa ajili ya kusoma, nahofia kwamba huenda wakaambukizwa virusi vya covid-19 na wakawapelekea wazazi wao. Zaidi ya wanafunzi 500 wanatafuta elimu Kenya na mnaelewa nchi hiyo ina idadi kubwa ya maambukizi," Macho alinukuliwa na gazeti la Daily Monitor.

Macho na wabunge wenzake walitoa malalamishi hayo wakiwa kwenye mkutano na waziri wa Elimu nchini Uganda John Munyingo ambaye ameahidi kutafuta suluhu kuhusiana madai hayo.

Shule nchini Uganda haswa kwa wanafunzi wa shule ya chekechea, darasa la kwanza, la pili na la tatu hazijafunguliwa kwa mwaka mmoja sasa kufuatia mlipuko wa virusi vya COVID-19.

Hii ilipelekea wazazi wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya na Uganda kuwatafutia shule humu nchini, hatua ambayo wabunge wanashikilia kwamba ni hatari.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke