Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yakana kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Tigray

Trigat Uganda Yakana Uganda yakana kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Tigray

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi nchini Uganda limekanusha ripoti kwamba linajaribu kuivuruga Ethiopia kwa kutoa mafunzo na kutoa msaada kwa chama cha Tigray People's Liberation Front - TPLF, ambacho kimekuwa na vita na serikali ya Ethiopia tangu 2020.

Ripoti hizo zilionekana kuibuka mara ya kwanza mnamo Meikatika mitandao ya habari ya nchini Ethiopia.

Msemaji wa Jeshi la Uganda Brigedia Felix Kulayigye alisema kupitia Twitter siku ya Jumapili kwamba madai ya majaribio ya Uganda kuyumbisha Ethiopia ni uzushi mtupu.

Makala ya kina ilionekana wiki iliyopita katika kituo cha mtandaoni kilichoko New Zealand, pamoja na orodha ya maafisa wakuu wa jeshi la Uganda na wengine kutoka katika vikosi vya usalama, ambao wanadaiwa kuongoza operesheni ya mafunzo katika wilaya ya kati ya Uganda ya Masaka.

Stakabadhi hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya wanajeshi 4000 wa Tigray walipaswa kupewa mafunzo katika vituo vinne tofauti nchini Uganda.

Ripoti hiyo inadai zaidi kwamba shughuli ya mafunzo inaungwa mkono na Marekani na Misri.

Mmoja wa maafisa wakuu waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni mtoto wa Rais na kamanda wa jeshi la nchi kavu la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye alituma ujumbe kwenye Twitter akiunga mkono vikosi vya Tigray, akiwataja kama "ndugu", mnamo 2021.

Bado haijabainika stakabadhi hiyo ni ya kweli au ni sehemu ya kampeni ya habari ghushi. Tovuti ya New Zealand, inayojulikana kama Scoop, ilisema haikuweza kuthibitisha chanzo au ikiwa maelezo hayo yalikuwa sahihi au la.

Lakini kuna baadhi ya vitu visivyoeleweka -Inamtaja James Kabarebe kuwa Waziri wa Ulinzi wa zamani nchini Uganda, lakini nchi hiyo haijawahi kuwa na waziri kwa jina hilo katika nafasi hiyo.

Brigedia Kulayigye pia alisema katika Twitter kwamba madai ya ushirikiano kati ya Uganda na Sudan Kusini katika operesheni hiyo si ya kweli, kwa sababu balozi wa Uganda nchini Sudan Kusini, ambaye anatajwa kuwa mratibu wa sehemu ya operesheni hiyo, hajawahi kukutana na jenerali wa Sudan Kusini aliyetajwa katika ripoti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live