Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yaidhinisha Covidex kutumika kutibu corona

Covidex Uganda yaidhinisha Covidex kutumika kutibu corona

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Dawa Uganda, David Nahamya amewaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina, sasa taasisi hiyo ya serikali imeidhinisha rasmi matumizi ya Covidex kwa ajili ya kusaidia kupambana na magonjwa ambukizi yanayotoka na na virusi.

Awali, mamlaka hiyo ilipiga marufuku matumizi ya dawa hiyo ya asili iliyozalishwa na timu ya wanasayansi wa nchi hiyo wakiongozwa na Prof. Patrick Ogwang wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbarara.

Hata hivyo licha ya marufuku hiyo wananchi wa Uganda waliendelea kuinunua kwa wingi pamoja na bei yake kuongezeka maradufu.

Chanzo: ippmedia.com