Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yafungua mpaka wake kwa wakimbizi wa DR Congo

MIPAKA.png Uganda yafungua mpaka wake kwa wakimbizi wa DR Congo

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uganda imefungua sehemu ya mpaka wake kwa maelfu ya wakimbizi wa kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliokuwa wamekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Karibu watu 3,000 walitoroka makwao mwezi Mei baada ya mapigano ya kijamii kuzuka katika mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.

Lakini hawakuweza kuvuka na kuingia Uganda kwa sababu ilikuwa imefunga mipaka yake mwezi Machi kama juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Uamuzi umefikiwa kwamba wakimbizi hao watawekwa karantini kabla ya kupelekwa kambini.

Hili litafanyika katika muda wa siku 14 katika kituo cha kuwatenga watu kilichopo kilomita 13 sawa na (maili nane) kutoka mpakani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa litawafanyia uchunguzi wa kimatibabu watu hao kubaini ikiwa baadhi yao wameambukizwa virusi vya corona.

Hii itasaidia kuamua ni lini wakimbizi watahamishwa hadi kambi ya wakimbizi.

Mipaka miwili katika wilaya ya Zombo nchini Uganda imefunguliwa Jumatano ili kuwawezesha wakimbizi kuingia nchini humu kwa siku tatu.

Uganda inawahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni 1.4 - wengi wao kutoka nchini Sudan Kusini, huku karibu asilimia 30 wakitokea DR Congo.

Mashirika yamezungumzia ugumu wa kuhakikisha hatua ya kutokaribiana inatekelezwa na usafi ya hali ya juu katika makazi ya wakimbizi, mwanahabari wa BBC Catherine Byaruhanga anasema.

Hadi kufikia sasa wakimbizi 52 wamepatikana na virusi vya corona nchini Uganda katika karibia 900 waliothibitishwa kupata maambukizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live