Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yaagiza dozi milioni mbili chanjo ya Covid-19

72cecb33cf6f7da0edb0aa387efb8116 Uganda yaagiza dozi milioni mbili chanjo ya Covid-19

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UGANDA imekuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuagiza chanjo ya Virusi vya Corona. Taifa hilo la tatu kwa ukubwa Afrika Mashariki, limeagiza dozi milioni mbili za chanjo ya Covid- 19.

‘’Wizara imeomba chanjo ya Covid-19 ya AstraZeneca kupitia shirika la Global Vaccine Alliance (GAVI) na kuwa mchakato uko kwenye hatua za mwishoni,’’ Ripoti ya tovuti moja ilimnukuu Mkurugenzi wa huduma za afya, Henry Mwebesa.

Aliongeza kuwa chanjo hiyo imeleta matumaini kwa kuwa imepatiwa idhini na Shirila la Afya Duniani. Alisema ni muhimu kufahamu kwamba chanjo inayopitishwa na Wizara ya Afya na WHO ndio inaweza kupewa kutumiwa na raia wa Uganda.

Uganda inatarajia kupokea dozi milioni mbili kutoka Gavi mwanzoni mwa mwaka 2021 lakini imetenga bajeti kwa ajili ya kununua dozi zaidi kwa ajili ya raia wa Uganda.

Kumekuwa na ongezeko la maambukizi kila siku wakati ambapo taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 14 mwezi Januari 2021. Mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa Uganda ina maambukizi ya watu 25,000.

Baadhi ya wanasiasa wameshutumiwa kwa kukiuka masharti ya kudhibiti virusi vya corona wakati wa kampeni.

Chanzo: habarileo.co.tz