Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda na DR Congo zakubaliana kuhusu usafiri bila visa

Uganda Na DR Congo Zakubaliana Kuhusu Usafiri Bila Visa Uganda na DR Congo zakubaliana kuhusu usafiri bila visa

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekubaliana kuondoa masharti ya visa ili kuwawezesha raia wa mataifa hayo mawili kusafiri bila visa.

Makubaliano hayo yanalenga kurahisisha harakati za watu na kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yanafuatia mazungumzo ya hivi karibuni kati ya maafisa wa nchi hizo mbili katika mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa miezi kadhaa amekuwa akitetea uingiaji wa visa bila malipo kati ya nchi hizo mbili.

"Kuvuka katika Afrika Mashariki kunapaswa kuwa bila gharama. Unalipa visa unapoenda Marekani, au Ulaya, lakini visa ya DR Congo?! Hiyo ni takataka. Ikiwa ni hivyo, nimeiondoa,” Rais Museveni alisema Desemba mwaka jana alipozindua kituo cha mpakani cha Mpondwe kwenye mpaka wa Uganda na DR Congo.

Mnamo Mei, alitoa wito kwa maafisa kutoka nchi zote mbili kuharakisha mchakato wa kuanzisha usafiri bila visa.

Maraia wa Uganda na DR- Congo hapo awali wamelalamika kuhusu kulipa ada kubwa Ya visa katika vivuko vya mpakani.

Chanzo: Bbc