Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kuzindua uchimbaji wake wa kwanza wa kisima cha mafuta

FnNleHUXkAAVcQH.jpeg Uganda kuzindua uchimbaji wake wa kwanza wa kisima cha mafuta

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la mafuta linalomilikiwa na serikali ya Uganda imesema itazindua uchimbaji wa kisima chake cha kwanza cha mafuta katika eneo la Kingfisher nchini humo hii leo.

Inatarajiwa kufikia 2025 mafuta yatatiririshwa katika mapipa bilioni 1.4 kutoka kwenye visima vya mafuta katika eneo la magharibiya kati.

"Leo tunaadhimisha hatua nyingine muhimu na kukaribia kupata mafuta kwa uzinduzi wa uchimbaji wa visima na uzalishaji wa mafuta eneo la Kingfisher," Mamlaka ya Petroli ya Uganda (PAU) imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuongoza hafla hiyo.

Eneo la mafuta la Kingfisher linaendeshwa na CNOOC ya Uchina, huku eneo la pili la mafuta la Tilenga likiendeshwa na Kampuni ya TotalEnergies ya Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live