Shirika la usimamizi wa mazingira nchini Uganda linasema litaanza kutoza faini kuanzia mwezi Aprili kwa madereva wanaoendesha magari ya kibinafsi bila ya kuwa na chombo cha kuhifadhia takataka.
Wahalifu watakabiliwa na faini ya juu zaidi ya hadi shilingi 6,000,000 za Uganda ($1,630), kwa mujibu wa mpango wa adhabu uliotangazwa Jumatano.
Waendeshaji magari wanaokataa kulipa faini watakabiliwa na mashtaka na kifungo au faini itakayoamuliwa na mahakama, shirika hilo lilisema katika taarifa.
Hivi sasa mabasi ya abiria yanayosafiri umbali mrefu nchini humo yanalazimika kuwa na chombo cha takataka.
Lakini ni hitaji jipya la chombo cha taka katika magari ya kibinafsi ambalo limepata usikivu wa Waganda, huku wengi wakiuliza kama kulikuwa na kiwango fulani cha kile kinachozingatiwa kama pa kuwekea taka.
"Mradi tu unatumia kitu ambacho hakiruhusiwi kuweka takataka zako, unapaswa kuwa sawa. Mifuko ya plastiki imepigwa marufuku," Naomi Karekaho, msemaji wa shirika hilo, aliiambia BBC.
Alisema shirika hilo litachukua ufafanuzi wa kile kinachozingatiwa kama chombo cha taka katika marekebisho yanayofuata.
"Kati ya adhabu zote za uvunjaji wa mazingira ambazo tulitangaza hii inaonekana kuwa imevutia watu wengi. Labda ni msisimko mkubwa wa kuwa na chombo cha taka kwenye gari," aliongeza