Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kupeleka wanajeshi Msumbiji

Wnajeshi Nug Msumbijii Uganda kupeleka wanajeshi Msumbiji

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema Uganda inaweza kupeleka kikosi kikubwa kusaidia kupambana na wanamgambo wa Kiislamu katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Mwenzake wa Msumbiji, Filipe Nyusi, yuko katika ziara ya siku tatu nchini Uganda ili kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Wanajeshi wa Uganda kwa sasa wametumwa Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi kutoka Rwanda na wengine kutoka jumuiya ya kikanda, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc), wanaisaidia Msumbiji kupambana na waasi.

Uganda hadi sasa imesaidia vikosi vya Msumbiji kwa zana za kijeshi. Utafiti wa shirika la Global Initiative Against Transnational Crime lenye makao yake makuu mjini Geneva ulionya mwezi Februari kwamba wanamgambo hao wamepanua operesheni zao ndani na nje ya Msumbiji licha ya kuingilia kati kwa vikosi vya kikanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live