Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kupeleka wanajeshi 1000 wa kulinda amani DR Congo

Uganda Kupeleka Wanajeshi 1000 Wa Kulinda Amani DR Congo Uganda kupeleka wanajeshi 1000 wa kulinda amani DR Congo

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Jeshi la Uganda linasema litatuma takriban wanajeshi wake 1000 katika ujumbe wa kulinda amani katika eneo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Vikosi vya Uganda tayari vinajishughulisha kivyake katika eneo hilo, katika misheni ya kivita pamoja na vikosi vya serikali ya Congo dhidi ya Allied Democratic Forces, kundi la waasi wa Uganda lenye kambi nchini humo.

Msemaji wa Jeshi, Jenerali Felix Kulaigye aliambia BBC kwamba wanajeshi hao wamekuwa mafunzoni tangu Juni katika wilaya ya Kiruhura, magharibi mwa Uganda.

Tangazo hilo linakuja siku chache baada ya nchi jirani ya Kenya kutuma kundi la pili la wanajeshi wake katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC kushiriki katika ujumbe wa kulinda amani wa kikanda uliokubaliwa mwezi Aprili na nchi saba za Afrika Mashariki ambazo DRC ni sehemu yake, kufuatia kuibuka tena kwa waasi wa M23.

Waasi wa M23 katika wiki za hivi karibuni wameendelea kusonga mbele kuelekea Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini huku wakielekea kuweka maeneo zaidi chini ya udhibiti wao.

Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao katika duru ya hivi punde ya mapigano. Siku ya Jumapili, viongozi wa Afrika Mashariki walitangaza kuwa mazungumzo yanayolenga kuleta amani mashariki mwa DRC yatafanyika mjini Nairobi mwezi huu.

Chanzo: Bbc