Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kujibu mapigo yatangaza kuzifungia bidhaa za Kenya

Trade Uganda kujibu mapigo yatangaza kuzifungia bidhaa za Kenya

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda inajipanga kuzuia baadhi ya bidhaa za kilimo ghafi zilizosindikwa za nchini Kenya na kudai kuwa inafanya hivyo ili kujibu hatua ambazo Kenya imezichukua kwa kuzuia na kupiga marufuku bidhaa za nchini Uganda.

Siku ya Jumatatu, Desemba 13, 2021, Baraza la Mawaziri la Uganda lilikubali pendekezo hilo la takriban miaka miwili, ambalo mara nyingi limekuwa likipingwa na Rais Yoweri Museveni.

Kulingana na maelezo yaliytolewa na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Rebecca Kadaga, yalilitaka Baraza hilo la Mawaziri kuiagiza wizara ya Kilimo ya nchini Uganda kubainisha na kuorodhesha bidhaa za Kenya ambazo zitapigwa marufuku na serikali hiyo ndani ya "muda mfupi."

“Tumekuwa wavumilivu kupita kiasi. Hapo awali, hatujarudiana, lakini sasa tunaenda. Hili limeendelea kwa muda mrefu sana na kwa muda mfupi wao pia wataelewa kile tunachopitia,” Kadaga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live