Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kuanzisha msako kuwabaini wanaokopesha bila Leseni

Uganda Sh Uganda kuanzisha msako kuwabaini wanaokopesha bila Leseni

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya udhibiti wa fedha nchini Uganda, imeanzisha mkakati wa kuwabaini wale wote wanaokopesha fedha pamoja na waofanya biashara pasipo kuwa na leseni.

Taarifa hii imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Peter Emong Ojulang, na kusema kuwa wamepata taarifa ya kuwepo kwa watu hao ambao wanaviunja sheria ya nchi.

Mkurugenzi huyo ametumia kifungu namba 84 cha masuala ya fedha katika katiba ya nchini humo kinacho kataza kuendesha shughuli za kifedha pasipo kuwa na usajili kamili.

"Mamlaka hii imetambua uwepo wa kampuni za kukopesha nchini zisizo na leseni, wanafanya biashara biashara zao kinyume cha sheria, wanawatumia wananchi wasiokuwa na vipato vya kueleweka hasa wale walio athirika na jangala UVIKO-19, wana wadanganya, tunawajulisha kuwa tumeanzisha mpango kazi wa kuwabaini" Mkurugenzi Peter Emong.

Aidha amewataka wananchi kufanya biashara na kampuni zilizosajiliwa, ili kuepuka vitendo hivyo vya uhalifu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live