Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda imesitisha safari za ndege kutoka India

UGANDAAA ED Uganda imesitisha safari za ndege kutoka India

Fri, 30 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng amesema Serikali imechukua hatua mbali mbali ili kuzuia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivyo .

Hakuna abiria kutoka India atakayeruhusiwa kuingia nchini humo bila kujali alikotokea na abiria wote waliopitia au kutoka India katika siku 14 zilziopita pia hawatakubaliwa kuingia nchini humo .

Wasafiri wote kutoka India wataaowasili Uganda kabla ya kuanza kutekelezwa kwa marufuku hiyo watatakiwa kuwa na cheti cha kuthibitisha kwamba wamepimwa na kupatikana bila virusi vya Corona katika kipindi cha saa 120 wakati sampuli zilipochukuliwa kutoka kwao.

Wizara ya Afya nchini Uganda imeongeza kwamba wote watakaowasili nchini humo kabla ya marufuku hiyo kuanza kutekelezwa watapimwa Corona pindi watakapowasili na watakaopatikana kuwa bila virusi hivyo watatakiwa kujitenga wenyewe na kisha kurejea kwa vipimo baada ya siku 5 hadi 10 .

Watakaopatikana na Corona watalazimika kuwekwa chini ya karantini ya serikali ambayo watagharamia wenyewe

Chanzo: ippmedia.com