Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Yakaribisha wakimbizi wa Afghanistan

Wakimbizi Pc Data Wakimbizi Afghanistan

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uganda imejiandaa kupokea wakimbizi 2,000 kutoka Afghanistan kufuatia machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.

Waziri wa Uganda anayehusika na masuala ya maafa na wakimbizi, Esther Anyakun amesema wamefikia uamuzi huo kufuatia ombi la serikali ya Marekani lililokubaliwa na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

"Tunatarajia kuwakaribisha kwa muda wakimbizi kutoka Afghanistan kabla hawajahamishwa na serikali ya Marekani. Hili ni ombi kutoka serikali ya Marekani kwenda kwa Rais wetu, tumeanza maandalizi jana,"

"Tunatarajia wanaweza kuja wakati wowote kwa kuwa watatua kwa dharura, wametuomba tuwapokee wakimbizi 2,000 na wataapokelewa kwa makundi,"

Ameongeza kuwa kundi la kwanza la wakimbizi wapatao 500 wa walitarajiwa kufika Agosti 16 lakini haikuwezekana.

Kulingana na taarifa ya serikali ya Uganda, gharama zote zitakazotumika kipindi wakimbikizi hao wakiwa nchini huwa zitalipwa na Marekani.

Wakimbizi hao watapewa makazi nchini Uganda kwa kipindi cha miezi mitatu na watafika katika makundi ya watu 500.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live