Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Wanafunzi 3 kati ya 6 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Jeshi Uganfda Uganda: Wanafunzi 3 kati ya 6 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Uganda limewaokoa wanafunzi 3 kati ya 6 waliokuwa wametekwa nyara na waasi wa kundi la ADF lenye makao yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi hao walivamia shule ya Lubirira huko magharibi mwa Uganda wiki iliyopita na kuuwa watu 42 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wenye umri mdogo. Haya ni kwa mujibu wa jeshi la Uganda. Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amesema kuwa wanafunzi watatu wameokolewa kati ya sita waliokuwa wametekwa nyara na waasi wa ADF wiki iliyopita huko Mpondwe.

Kulayigye ameongeza kuwa, mwanamke na watoto wake wawili ambao walitekwa nyara nje ya shule hilo pia wameokolewa kutoka mikononi mwa waasi. Amesema waasi wawili wameuawa na jeshi la Uganda limenasa bunduki mbili. Ijumaa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita waasi wa kundi la ADF lenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) walishambulia shule ya sekondari ya Lhubirira huko Mpondwe katika mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi wa ADF waliiingia katika bweni la wanafunzi wa kiume, na kuanza kuwapiga risasi,kuchoma moto bweni lao na kumchoma moto karibu kila mmoja. Baada ya hapo, waasi hao waliiingia katika bweni la wasichana na kuanza kuwauwa kwa mapanga. Shambuylio hilo limetajwa kuwa la kutisha zaidi kuwahi kushuhudiwa huko Uganda katika miongo kadhaa.

Miili mingi iliyookotwa kutoka kwa bweni la wavulana iliungua moto kiasi cha kutotambulika;ambapo mamlaka husika za Uganda zimetumia vipimo vya DNA vilivyo na sampuli zilizowasilishwa na wazazi wa wanafunzi hao ili kuwatambua. ADF, kundi la zamani la waasi wa Uganda, linaendesha harakati zake katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; na katika miongo miwili iliyopita limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia huko Kongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live