Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Mahakama yapinga rufaa ya wapenzi wa jinsia moja kutaka usajili

Uganda: Mahakama Yapinga Rufaa Ya Wapenzi Wa Jinsia Moja Kutaka Usajili Uganda: Mahakama yapinga rufaa ya wapenzi wa jinsia moja kutaka usajili

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Uganda Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja lililotaka usajili wa serikali, na kuamua kwamba kundi hilo lina lengo la kuendeleza shughuli “haramu”.

Mahakama ya rufaa ilisema usajili wowote wa kundi la Sexual Minorities Uganda (SMUG) ni kinyume na maslahi ya umma na sera ya kitaifa.

Walalamishi walitaka jina hilo lisajiliwe “ kwa madhumuni ya kuimarisha haki za ngono za watu walio wachache wanaojulikana kama LGBTQ,” aliamua Jaji Catherine Bamugemereire kwa niaba ya jopo la majaji watatu.

Wanaharakati walikuwa wanakata kusajili SMUG kama kampuni ndogo ili kuiwezesha kufanya kazi kihahali nchini Uganda, ambapo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vimeharamishwa.

Chanzo: Bbc