Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Mahakama kutathimini ushahidi kuhusu sheria mapenzi ya jinsi moja

Uganda: Mahakama Kutathimini Ushahidi Kuhusu Sheria Mapenzi Ya Jinsi Moja Uganda: Mahakama kutathimini ushahidi kuhusu sheria mapenzi ya jinsi moja

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Kikatiba nchini Uganda imepokea ushahidi uliowasilishwa na pande mbili katika kesi ya kupinga sheria dhidi ya mapenzi ya jinsi moja nchini humo.

Mahakama hiyo sasa itaangalia na kutahmnini ushahidi wa kila upande na kutangaza tarehe ya kutoa hukumu.

Kesi ya kupinga sheria dhidi ya mapenzi ya jinsi moja iliwasilisha na watetezi wa haki za kibinadamu, asasi za kiraia pamoja na watu mbali mbali wakidai sheria hiyo inakiuka haki za kibinadamu.

Lakini upande wa utetezi ukiongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali unasema sheria hiyo inalenga kulinda familia na maadili ya utamaduni wa nchi hiyo.

Sheria hiyo ilitiwa saini na rais Yoweri Museveni mnamo tarehe 26 Mei mwaka huu na hivyo kuwa sheria kamili. Moja ya vipegele vitatu katika sheria hiyo ni adhabu ya kifungo cha maisha na adhabu ya kifo kwa wanaopatikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsi moja nchini Uganda.

Tangu kupitishwa kwake, sheria hiyo imekosolewa na nchi za magharibi.

Marekani tayari imewawekea vikwazo baadhi ya maafisa katika serikali ya Uganda kwa kutuhumiwa kuminya haki za kibindamu na nchi hiyo pia imeondolewa kutoka kwenye mpango maalumu wa kibiashara wa AGOA.

Lakini hii sio mara ya kwanza mahakama ya Kikatiba kusikiliza kesi kuhusu sheria dhidi ya mapenzi ya jinsi moja, mnamo Agosti 2014, mahakama hiyo hiyo ilibatilisha sheria kupinga mapenzi hayo kwa misingi ya utaratibu kutokana Akidi kutotimia kwa wabunge kupitisha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live