Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Idadi ya waliofariki kwa maporomoko ya ardhi eneo la kutupa taka yafikia 21

Uganda: Idadi Ya Waliofariki Kwa Maporomoko Ya Ardhi Eneo La Kutupa Taka Yafikia 21.png Uganda: Idadi ya waliofariki kwa maporomoko ya ardhi eneo la kutupa taka yafikia 21

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Takriban watu 21 hadi kufikia sasa wamethibitishwa kufariki dunia baada ya maporomoko ya ardhi katika eneo kubwa la kutupa taka katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Waokoaji wanaendelea kuchimba uchafu huo kwa matumaini ya kupata manusura zaidi baada ya maporomoko hayo yaliyofuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa wiki kadhaa.

Eneo la kutupa takataka la Kiteezi lenye ukubwa wa ekari 36 (hekta 14) ndilo pekee linalohudumia Kampala nzima, jiji ambalo linakadiriwa kuwa na watu milioni nne.

Meya wa Kampala Erias Lukwago aliliambia shirika la habari la AFP "ni janga [ambalo] lazima lingetokea", na kwamba "wengi, wengi zaidi bado wanaweza kuwa bado wamezikwa".

Chanzo: Bbc