Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Hatuhitaji fedha za wanaoshabikia ushoga

Spika Uganda Uganda Uganda: Hatuhitaji fedha za wanaoshabikia ushoga

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge la Uganda amekosoa tabia ya madola ya Magharibi ya kutoheshimu tamaduni za watu wengine na badala yake kung'ang'ania misimamo yao kama uozo wa ushoga na ubaradhuli.

Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among amesema hayo katika ujumbe aliotuma jana Jumanne kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusitiza kuwa, nchi hiyo ya Afrika Mashariki katu haitaunga mkono vitendo vichafu vya mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Amebainisha kuwa, Bunge la Uganda kuanzia leo Machi Mosi litaanza kujadili muswada wa marekebisho ya sheria ya kupambana na ushoga na kueleza kuwa, lengo la sheria hiyo ni kuwalinda Waganda dhidi ya fitina ya mashoga na waungaji mko wao.

Among ameeleza bayana kuwa, "Sheria Dhidi ya Ushoga itawasilishwa kesho (leo Jumatano); hatufurahii namna thamani (za kitamaduni) za Uganda zinavyosambaratishwa. Hatuhitaji pesa zao, tunahitaji utamaduni wetu."

Rais Yoweri Museveni wa Uganda wiki iliyopita, alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, nchi yake haitaunga mkono vitendo hivyo vichafu vya mapenzi ya watu wenye jinsia moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live