Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: 17 wafariki kwa ugonjwa wa kimeta

Kifo Kifo Mauiaji.png Uganda: 17 wafariki kwa ugonjwa wa kimeta

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 17 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kimeta katika wilaya ya kusini mwa Uganda mwezi huu wa Novemba.

Hayo yamethibitishwa na afisa wa eneo hilo ambaye ameviambia vyombo vya habari kuwa "hali hiyo imedhibitiwa".

Afisa wa afya wa wilaya hiyo, Dk. Edward Muwanga, ameiambia AFP kwamba katika wilaya ya Kyotera, kusini mwa Uganda, takriban kilomita 180 kutoka mji mkuu, Kampala, "watu 17 wamefariki dunia" mwezi Novemba kutokana na ugonjwa wa kimeta na kwamba "wanashukiwa kula nyama kutoka kwenye shamba ambako wanyama walikuwa wameambukizwa ugonjwa huo." Daktari Muwanga ameongeza kuwa: "Tunafanya kazi na timu za Wizara ya Afya ya Kampala na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambao wanasaidia kudhibiti kikamilifu hali hiyo.

Watu 17 wameaga dunia kwa ugonjwa wa kimeta, Uganda Mwezi Julai mwaka huu Nigeria pia alithibitisha rasmi kesi ya kwanza ya ugonjwa wa kimeta kupitia taarifa iliyotiwa saini na Afisa Mkuu wa Mifugo wa nchi hiyo, Columba Vakuru.

Kimeta ni ugonjwa mbaya wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria aina ya Bacillus Anthracis. Ugonjwa huu huwaathiri binadamu na wanyama, ikiwa ni pamoja na wanyama wa porini na wale wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama ng'ombe, kondoo, mbuzi, nk.

Baadhi ya dalili za kimeta ambazo huwa nazo mtu aliyeambukizwa ni homa na baridi, maumivu ya kichwa, kuvimba kwa tezi za shingo au shingo lenyewe, maumivu ya koo, kumeza kwa uchungu, kutapika n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live