Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa yakiri kudaiwa na Afrika

Macron 1 Ufaransa yakiri kudaiwa na Afrika

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa nchi yake inadaiwa na baadhi y nchi barani Afrika na tayari wameshajipanga kuanza mchakato wa kulipa madeni hayo.

Kiongozi huyo amesema hayo katika mkutano wa kwanza wa Ufaransa na Afrika usio wahusisha wanasiasa, na kusisitiza kuwa Mahusiano baina ya Ufaransa na Afrika kipindi cha ukoloni hayakuwa mazuri kwa pande zote mbili na kuwa hali hiyo inapaswa kuchukuliwa kama funzo baina yao.

"Ufaransa inalo deni kubwa kwa Afrika, ni lazima tutafute njia bora za kukamilisha malipo haya" Amesema Rais huyo.

Rais huyo ametoa kauli hiyo mbele ya wawakilishi zaidi ya 5,000 kutoka bara la Afrika hasa katika nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa.

Ameongeza kusema kuwa, ni muhimu kwao kulipa madeni hayo ili kuimarisha mahusiano na nchi zilizoathiriwa na utawala wa kikoloni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live