Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa yafunga ubalozi wake nchini Niger

FRANCEE ET ALLIES Ufaransa yafunga ubalozi wake nchini Niger

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Ufaransa umetangaza kufunga ubalozi wake nchini Niger kwa muda usiojulikana kwani haiwezi tena kutekeleza majukumu yake kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliofanywa nchini humo mwezi Julai.

Barua kwa wafanyakazi kutoka kwa balozi ilisema mamlaka imeshindwa kujibu maombi ya mara kwa mara ya kuruhusu ubalozi kufanya kazi zake kama kawaida nchini Niger.

Ufaransa na Niger zilikuwa washirika katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika eneo hilo, lakini uhusiano ulidorora baada ya mapinduzi.

Utawala wa kijeshi ulitupilia mbali mikataba ya ulinzi na kuamuru balozi na wanajeshi wa Ufaransa kuondoka.

Chanzo: Bbc