Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa yaendelea kuondoa wanajeshi wake nchini Mali

Ufaransa Mali Jeshi Ufaransa yaendelea kuondoa wanajeshi wake nchini Mali

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ufaransa imeendelea kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali, sambamba na kukabidhi kambi yake ya kijeshi ya Menaka kwa vikosi vya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Mali imesema ukabidhianaji huo umefanyika kwa utaratibu maalumu, salama na wenye uwazi, na ni sehemu ya mpango uliopasishwa na Rais wa Ufaransa mwezi Februari mwaka huu, wa kuangaliwa upya Operesheni ya Barkhane iliyoanza mwaka 2014.

Haya yanajiri mwezi mmoja baada vikosi vya usalama vya Mali kugundua makaburi ya halaiki waliyozikwa ndani yake raia wa nchi hiyo katika kituo kingine cha askari hao wa Ufaransa mjini Gossi.

Jeshi la Ufaransa lililazimika kuondoka kwenye kambi hiyo mwezi Februari mwaka huu baada ya jeshi la Mali kumlaumu mkoloni huyo mkongwe wa Ulaya kwamba anashiriki katika kuharibu usalama wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Serikali ya kijeshi nchini Mali imechukua uamuzi wa kukata rasmi ushirikiano wa kijeshi na Paris kutokana na kuwa askari wa Ufaransa wamekuwa wakikiuka mamlaka ya kujitawala nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kwa mara kadhaa kumejiri maandamano makubwa dhidi ya Ufaransa nchini Mali ambapo wananchi wamekuwa wakishinikiza serikali ya nchi hiyo isitishe kikamilifu ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live