Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa kutoa dozi millioni 120 kwa nchi masikini

Chanjo 7 Chanjo

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Ufaransa imeahidi kuzidisha mara mbili idadi ya Dozi ya chanjo za virusi vya Corona kufikia milllion 120 kwa lengo la kusaidia nchi zenye uhitaji. kuweza kusaidia nchi zenye uhitaji .

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa ahadi hiyo Septemba 25,katika tamasha la Global Citizen lililofanyika nchini humo huku akisema wanatoka kwenye kutoa Dozi millioni 60 mpaka kufikia dozi millioni 120 kwa nchi zenye uhitaji.

Katika kufanikisha suala hili, taifa hilo limenuia kutoa asilimia 20 ya fedha itakazo pkea kutokakatika Shirik la Fedha Duniani IMF, kwa ajili ya kuwezesha zoezi la utoaji wa chanjo hiyo.

Hata hivyo Serikali ya Marekani ilitangaza kuzidisha idadi ya dozi za Chanjo ya Corona hdi kufikia bilioni 1.1 kwa nchi zenye uhitaji.

Hatua hii inaungwa mkono na nchi za bara la ulaya ambazo zimepanga kutoa dozi milioni 500, sambamba na China ambayo imeahidi kutoa jumla ya dozi bilioni 2 mwishoni mwa mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live