Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi waendelea kichwa cha mtu bungeni

Adad1d8b48395e415aaf90ec4509ae9b Uchunguzi waendelea kichwa cha mtu bungeni

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

POLISI nchini Uganda wanaendelea kumhoji mwanaume aliyekamatwa kwenye majengo ya Bunge akidai kumpelekea Spika wa Bunge zawadi ambayo iligunduliwa ni kichwa cha mtu.

Tukio hilo lililotokea wiki iliyopita, liliwashtua watu wengi na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike. Habari zinasema, mwanamume huyo ambaye inasemekana alijifanya msichana, aliwasili kwenye majengo ya Bunge na kutaka kuwasilisha zawadi hiyo kwa Spika.

Naibu Msemaji wa Polisi Kanda ya Mji wa Kampala, Luke Owoyesigire, alisema polisi wanachunguza kama kichwa hicho ni cha mwili wa mtoto uliopatikana katika kichaka mjini Masaka, umbali wa kilomita 130 kutoka Kampala.

Tukio la mtu huyo kuwasilisha kichwa cha mtu kwenye majengo ya Bunge limekuwa gumzo kubwa linalotawala kwa sasa mjini Kampala na sehemu mbalimbali za Uganda.

Baadhi ya watu wanalihusisha tukio hilo na ushirikina, wakidhani kuwa ni mojawapo ya visa vya kafara za watoto zinazofanywa kila mara na baadhi ya watu wanaoendekeza imani hizo.

Tukio hilo si la kwanza, kwani kuna wakati kundi la vijana lilitupa kwenye lango la Bunge hilo nguruwe wadogo wakiwa wamepakwa rangi ya njano ya chama tawala.

Chanzo: habarileo.co.tz