Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi waanza ajali ya moto iliyouwa watu 77 Afrika Kusini

Ajali Moto Afrika Kusini Uchunguzi waanza ajali ya moto iliyouwa watu 77 Afrika Kusini

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchunguzi kuhusu ajali ya moto mjini Johannesburg Afrika Kusini ulianza jana Alkhamisi kwa lengo la kubaini wahusika wa tukio hilo lililosababisha vifo vya watu 77.

Uchunguzi huo utaangazia pia magenge ambayo yanateka majengo yaliyotelekezwa katikati ya jiji na kuyakodisha kinyume cha sheria.

Moja ya maafa mabaya sana kutokea katika kumbukumbu ya maisha katika kitovu cha uchumi wa Afrika Kusini, ni moto huo ambao ulizuka Agosti 31 katika jengo bovu lililojaa wahamiaji wa kigeni. Waathiriwa wengi waliungua kiasi cha kutotambulika.

Ripoti za awali zilionyesha kuwa, wakaazi wa jengo hilo lililokumbwa na moto mjini Johannesburg walikuwa wahamiaji wa mataifa mbalimbali. Baadhi ya maiti za wahanga wa ajali ya moto nchini Afrika Kusini

Taarifa za ndani zilisema kuwa eneo lilipo jengo hilo ni kitongoji cha ndani ya jiji ambacho kina sifa mbaya kwa majengo 'yaliyotekwa nyara', neno linalotumiwa nchini Afrika Kusini likimaanisha majengo yaliyochukuliwa kinyume cha sheria na wahamiaji wasio na vibali.

Kufuatia moto huo, raia wengi wa Afrika Kusini kwenye mitandao ya kijamii walilaani mashambulizi ya mtandaoni ya chuki dhidi ya wageni ambayo baadhi wameyafanya dhidi ya waathiriwa na manusura wa moto huo.

Wakazi wa majengo kama hayo pia hutegemea kuunganishiwa umeme kinyume cha sheria, majiko ya gesi na wakati umeme unapokatika nchini humo hutumia mishumaa ambayo yote ni hatari sana na kusababisha moto kuzuka.

Haijafahamika uchunguzi huo utakamilika lini na ripoti kamiili kutolewa kuhusiana na mkasa huo wa moto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live