Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi unaonyesha jambazi alipiga simu kudhibitisha amemuua mwanahabari

Crime Scene Decoration  Mw 133583 2 Uchunguzi unaonyesha jambazi alipiga simu kudhibitisha amemuua mwanahabari

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Betty Barasa aliuawa usiku wa Jumatano, Aprili 7, na genge la wanaume watatu ambao walimshambulia alipowasili nyumbani kutoka kazini

- Maafisa wa polisi walisema kwamba jambazi huyo aliyempiga risasi alipiga simu ya kutatanisha kudhibitisha alikuwa amemuua

- Makachero wanasema huenda jangili huyo alikuwa akisubiri amri kutoka mahali kabla ya kutekeleza unyama huo

Taarifa nyingine imeibuka kuhusu jinsi jambazi alipiga simu ya kutatanisha baada ya kumpiga risasi Betty Barasa, mhariri wa video katika Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) na vile vile mwandishi wa habari.

Barasa aliuawa kwa kupigwa risasi jioni Jumatano, Aprili 7, nyumbani kwake huko Ngong na genge la watu watatu ambao walimshambulia mara tu alipofika nyumbani.

Kulingana na ripoti ya Shahidi News, maafisa wa polisi walisema hata kabla ya jangili kumuua, "huenda kulikuwepo na mtu kwenye simu aliyekuwa akitoa amri."

Haya yanajiri wakati maafisa wa polisi wamekaza kamba katika kufichua kiini cha maujai ya kinyama ya Barasa.

Inasemekana mwanahabari huyo aliwasili nyumbani kwake mwendo wa saa mbili na dakika 20 usiku wakati genge la majambazi lililokuwa kwenye lango kuingia kwa lazima katika boma lake baada ya mjakazi wake kufungua lango.

Kisha genge hilo lilimfuata hadi eneo la kuekeza gari na kumshurutisha awapeleke kwake ambapo wanawe na mume wake walikuwa.

Wezi hao walimuitisha pesa na mali yake nyingine yenye thamani wakitaka awaongoze hadi kwenye chumba chake cha kulala.

Mmoja wa majambazi hao ambaye aliandamana naye chumbani alitofautiana na Betty na kisha alimfyatulia risasi licha ya kumuomba amuwachie uhai wake.

Betty alipigwa risasi mara mbili kichwani kabla ya majambazi hao kuondoka na kipatakilishi yake na simu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke