Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi kufanyika mauaji ya raia Burkina Faso

Burkina Faso Magaidiii 53 Uchunguzi kufanyika mauaji ya raia Burkina Faso

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya umesisitiza juu ya kufanyika uchunguzi wa mauaji ya raia 100 nchini Burkina Faso.

Jarida la June Afrique liliripoti Jumatatu iliyopita kuwa raia 100 wakiwemo wanawake na watoto kadhaa waliuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Zaongo nchini Burkina Faso.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Josep Borrell, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, alisema Jumapili katika taarifa yake kwamba: Umoja wa Ulaya unaitaka serikali ya mpito ya Burkina Faso kufanya utafiti na kuwa wazi kuhusu mauaji ya raia 100 katika nchi hiyo.

Amewataka viongozi wa Burkina Faso kuonyesha uwajibikaji wao kuhusiana na mauaji hayo. Askari Jeshi la Burkina Faso

Mkazi wa eneo hilo ambaye jina lake halikutajwa anasema: Mauaji haya yalijiri siku mbili baada ya mapigano kati ya vikosi vya usalama vya Burkina Faso na magaidi.

Ameongeza kuwa ni vigumu kubaini idadi kamili ya waliofariki kwa sababu miili yao ilizikwa mara moja baada ya tukio hilo.

Rais Ibrahim Traore, wa serikali ya mpito ya Burkina Faso, ameonya kuhusu uwezekano wa kuhusishwa jeshi na mauaji hayo kabla ya kufanyika utafiti.

Nchi ya Burkina Faso imekuwa ikitawaliwa na serikali ya mpito tokea mapinduzi ya Septemba 2022.

Ghasia na machafuko ya magaidi ulioanza mwaka 2015 nchini Mali pia umeenea hadi Burkina Faso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live