Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchumi Rwanda kukua kwa asilimia 5.1

8f36ae9db4225b15140d9e9f8786cefa.jpeg Uchumi Rwanda kukua kwa asilimia 5.1

Tue, 18 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UCHUMI wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.1 mwaka huu baada ya kushuka kwa asilimia 3.4 mwaka jana kutokana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19.

Ukuaji huo unatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 7.0 mwaka 2022 na wastani wa asilimia 7.8 mwaka 2023/24 kutokana na shughuli za kilimo, viwanda, madini na ujenzi.

Waziri wa Fedha, Richard Tushabe alisema hayo bungeni wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22.

Alisema Rwanda inapanga kuongeza matumizi katika mwaka wa fedha kuanzia Julai Mosi kwa asilimia 10 hadi faranga trilioni 3.807 (sawa na dola za Marekani bilioni 3.82 ).

Alisema wafadhili watafadhili asilimia 16 ya bajeti hiyo na fedha nyingine zitatokana na mapato ya ushuru na madeni,.

Alisema serikali itakopa faranga bilioni 651.5 katika mashirikia ya kimataifa, huku deni la taifa likielezwa kupanda kwa asilimia 13 kwa sababu ya kukopa kwa lengo la kupambana na athari za covid-19, alisema.

Deni lote la umma nchini lilipanda hadi asilimia 71 ya Pato la Taifa mwishoni mwa mwaka jana na linakadiriwa kufikia asilimia 79.7 mwishoni mwa mwaka huu.

"Tunakubali kwamba viwango vya deni vimepanda lakini bado hatujafikia kiwango kibaya cha deni," alisemaTushabe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz