Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ucheleweshaji wa uchaguzi wa Senegal watajwa kuwa kinyume cha sheria

Ucheleweshaji Wa Uchaguzi Wa Senegal Watajwa Kuwa Kinyume Cha Sheria.png Ucheleweshaji wa uchaguzi wa Senegal watajwa kuwa kinyume cha sheria

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa mwezi huu nchini Senegal ni kinyume na katiba ya nchi hiyo, mahakama ya juu ya nchi hiyo imeamua.

Mahakama ya Kikatiba ilibatilisha agizo la Rais Macky Sall na mswada tata uliopitishwa na bunge kusogeza kura hiyo hadi Desemba.

Maandamano makubwa yameikumba nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ambayo wakati mmoja ilichukuliwa kuwa ngome ya demokrasia katika eneo hilo.

Wapinzani walisema ni sawa na "mapinduzi ya kitaasisi".

Bw Sall alikuwa ametangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa sababu ya kile alichodai kuwa ni wasiwasi kuhusu kustahiki kwa wagombea wa upinzani.

Pendekezo lake lilikuwa limeungwa mkono na wabunge 105 kati ya 165. Hapo awali ilipendekezwa kuahirishwa kwa miezi sita, lakini marekebisho ya dakika za mwisho yalizidisha muda huo hadi miezi 10, au tarehe 15 Desemba.

Bw Sall alikuwa amekariri kwamba hakuwa na mpango wa kuwania wadhifa huo tena. Lakini wakosoaji wake walimshutumu kwa kujaribu kung'ang'ania mamlaka au kushawishi matokeo ya atakavyorithiwa .

Wagombea wa upinzani na wabunge, ambao walikuwa wamewasilisha pingamizi kadhaa za kisheria kwa mswada huo, huenda wakahisi kupewa afueni na uamuzi wa mahakama Alhamisi jioni.

Khalifa Sall, mpinzani mkuu na meya wa zamani wa mji mkuu wa Dakar, ambaye hana ujamaa na rais, alitaja kucheleweshwa kwa uchaguzi kama "mapinduzi ya kikatiba" wakati Thierno Alassane Sall, mgombea mwingine, ambaye pia hana uhusiano wowote,na rais aliitaja hatua hiyo kama "uhaini mkubwa" .

Chanzo: Bbc