Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ucheleweshaji wa malipo wazua mjadala katika mazungumzo ya amani ya DR Congo

Ucheleweshaji Wa Malipo Wazua Mjadala Katika Mazungumzo Ya Amani Ya DR Congo Ucheleweshaji wa malipo wazua mjadala katika mazungumzo ya amani ya DR Congo

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Kufungwa rasmi kwa mazungumzo ya amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Nairobi siku ya Jumatatu kuliahirishwa dakika za mwisho baada ya baadhi ya wajumbe kutoka nje wakipinga kutolipwa posho na masuala mengine.

Mazungumzo hayo ya wiki moja yaliyoongozwa na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta yaliwaleta pamoja wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makundi makubwa ya waasi, manusura wa mzozo huo na jumuiya za kiraia kwa mara ya kwanza katika mchakato huo.

Bw Kenyatta, ambaye aliratibiwa kutoa baadhi ya matamko mwishoni mwa mkutano huo, aliwasihi wajumbe hao wamruhusu kuahirisha mkutano huo hadi Jumanne anapojaribu kushughulikia maswala yaliyoibuliwa.

"Tunajua tuna fedha za kutosha na najua kwa sababu nilikuwa mmoja wa watu waliosaidia kutafuta fedha kusaidia kuleta amani DRC," Kenyatta alisema.

Aliwaonya waandaaji wa mazungumzo hayo kuwa kushindwa kutoa fedha hizo kama ilivyopangwa mapema kutaleta madhara.

Mazungumzo hayo yanalenga kuunda mifumo ya kurejesha amani mashariki mwa DR Congo, ambako zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanapigana.

Chanzo: Bbc