Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#UchaguziKenya: William Ruto apiga kura yake

Ruto Kura William Ruto apiga kura yake

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais na Mgombea urais nchini Kenya kupitia kwa chama cha United Democratic Alliance -UDA, William Ruto amepiga Kura mapema leo wakati wananchi wa taifa hilo wakiamua nani anastahili kurithi mikoba ya Rais Uhuru Kenyatta.

Ruto anashindana kwa ukaribu na Waziri Mkuu wa zamani Bwana Raila Odinga wa Azimio la Umoja.

’Ninajisikia vizuri kuwa baada ya miezi mingi ya kufanya kampeni na kuuza ajenda yetu, na leo asubuhi nimepiga kura yangu’.’ Dkt Ruto alisema.

Ametoa wito kwa raia kufanya uchaguzi kwa amani ili taifa lisonge mbele kwa njia ya demokrasia.

Aliongeza: ‘’Kila mtu hapa anataka mchakato wa amani. Ombi letu kabla ya kupiga kura lilikuwa kuhusu kuwa na uchaguzi wa amani. Pia nina furaha kwamba uchaguzi huu wa kihistoria utaleta enzi mpya kwa nchi. Nataka kuhimiza mchakato wa amani.’’

William Ruto anawania urais kwa mara ya kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: