Raia 11 wa Kenya wamesema uapisho wa mgombea Urais wa Chama cha UDA, William Ruto na Rigathi Gachagua utakua ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi yao hivyo kuwasilisha ombi katika Mahakama ya Juu nchini humo kupitia wakili wao Kibe Mungai, kuzuia kuapishwa kwao iwapo watachaguliwa katika Uchaguzi wa leo Agosti 9, 2022.
Raia 11 wa Kenya wamesema uapisho wa mgombea Urais wa Chama cha UDA, William Ruto na Rigathi Gachagua utakua ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi yao hivyo kuwasilisha ombi katika Mahakama ya Juu nchini humo kupitia wakili wao Kibe Mungai, kuzuia kuapishwa kwao iwapo watachaguliwa katika Uchaguzi wa leo Agosti 9, 2022. Wamefafanua kuwa kwa kuzingatia masharti ya Sura ya Sita ya Katiba, kuapishwa kwa wagombea hao na kushika madaraka itakuwa ni ukiukwaji wa wazi wa Ibara ya 3, 4 na 10 ya Katiba, kwa kuwa wawili hao hawakidhi vigezo vya uadilifu kama ilivyobainishwa katika Katiba hiyo.