Mgombea urais wa Kenya kupitia muungano wa Kenya Kwanza, William Ruto amewapongeza wagombea wote waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022 ukihusisha uchaguzi wa Rais, wabunge na magavana.
Ruto ambaye pia ni Naibu wa Rais, ametoa pongezi hizo wakati shughuli ya kuhesabu na kuhakiki kura za urais ikiendelea huku matokeo ya awali yakionyesha mchuamo mkali kati yake na Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga.
Mwanasiasa huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwapongeza washindi hasa wanawake ambao wamechaguliwa na kuwatakia heri katika majukumu yao mapya.
“Pongezi kwa washindi wote wa uchaguzi. Kipekee, tunasherehekea wanawake wengi ambao wamevunja vizuizi vya kupanda ngazi ya kisiasa. Kila la heri mnapoanza majukumu yenu mapya. Hustlers wanawategemea,” ameandika Ruto.
Katika uchaguzi huo huo, wanawake wameonekana kufanya vizuri katika nafasi za ugavana na ubunge ukilinganisha na ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2017. Ushiriki wao kwenye uchaguzi wa mwaka huu, umeongezeka zaidi.
IEBC yapunguza kura 10,000 za Ruto
Advertisement