Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#UchaguziKenya: Muuza Mkaa amwangusha Naibu Spika matokeo ya Ubunge

Alfred Mutai.jfif Alfred Mutai

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Diwani wa Wadi ya Sirikwa (MCA), Alfred Mutai amenyakua kiti cha ubunge jimbo la Kuresoi Kaskazini katika uchaguzi uliofanyika Jumanne, Agosti 9, 2022.

Mutai, ambaye alikuwa akiwania kwa tikiti ya Chama cha UDA, alipata kura 25,365, na kumshinda mshindani wake wa karibu, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Cheboi ambaye alitarajia kutetea kiti hicho. Cheboi alipata kura 20,395.

Hadithi ya Alfred Mutai ni ya kipekee akiwa amepitia visa hadi kuiona neema. Mzaliwa huyo wa Kaplong, Kaunti ya Bomet, alilazimika kujishughulisha na biashara tofauti ikiwa ni pamoja na kuchoma makaa kinyume cha sheria ili kujipatia mahitaji yake ya kila siku baada ya kuwapoteza wazazi wake mwaka wa 2001 akiwa kidato cha kwanza.

Kulingana na Mutai, ambaye ni mtoto wa nne kati ya watoto tisa, alilazimika kuhangaika kati ya kufanya kazi kama mhudumu na kuchoma makaa katika msitu wa Kuresoi kinyume cha sheria ili kupata pesa ya kulipa ada ya shule.

Una maoni Usisite kutuandikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: