Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#UchaguziKenya: Mbunge anayesakwa kwa mauaji ajisalimisha

Mbunge Asakwa Ajisalimisha.png #UchaguziKenya: Mbunge anayesakwa kwa mauaji ajisalimisha

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: Radio Jambo

Mbunge wa Kimilili kupitia chama cha UDA, Didmus Barasa hatimaye amejisalimisha kwa vyombo vya usalama, siku moja tu baada ya kitengo cha upelelezi wa jinai DCI kutangaza msako dhidi yake kwa tuhuma za mauaji ya mlinzi wa mshindani wake wa kisiasa, Brian Kahemba.

Alhamisi, DCI ilitoa taarifa kwa umma kwamba ilikuwa imempa Barasa chini ya saa sita tu kujisalimisha kwenye mikono salama ya kisheria la sivyo msako mkali dhidi yake ungeanzishwa na kumtia mbaroni.

"Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai inamuonya Mhe Didmus Barasa, ambaye amejificha baada ya mauaji ya kikatili ya Brian Olunga, kujisalimisha kwa kituo cha polisi kilicho karibu ndani ya saa 6 zijazo. Mhe Barasa, anasakwa kwa mauaji ya Brian, ambaye alimpiga risasi paji la uso na kumuua papo hapo, mnamo Jumanne, Agosti 8, eneo la Chebukwabi huko Kimilili, kaunti ya Bungoma," sehemu ya ripoti hiyo ya DCI ilisema.

Barasa ambaye alitangazwa kushinda wadhfa wa ubunge kimilili kwa mara ya pili alisemekana kutorokea kusikojulikana mnamo Jumanne usiku baada ya kumpiga risasi mlinzi wa mshindani wake ambaye walizozana katika kituo kimoja cha kupigia kura.

Baada ya DCI kutema moto huo, mwanasheria wa barasa, Wakili Khaminwa alielekea mahakamani kutaka mteja wake kupewa dhamana ili kesi hiyo kuendelea pindi atakapojisalimisha.

Barasa alitetea kiti chake kupitia tikiti ya UDA ila baada ya kutangazwa, ajenti wake alinyimwa cheti chake huku msimamizi wa uchaguzi katika kaunti hiyo alikataa ombi hilo la wakala wake na kumtaka Barasa mwenyewe kujisalimisha na kukabidhiwa cheti hicho cha ushindi.

Chanzo: Radio Jambo
Related Articles: