Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi wa Rais Januari 2021

C0313528257bc0056268f33c63542d02 Uchaguzi wa Rais Januari 2021

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TUME ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi wa Rais kufanyika Januari 14 mwakani.

Taarifa ya tume hiyo imeeleza kuwa wagombea urais 11 walioteuliwa kugombea nafasi hiyo wataanza kampeni Novemba 19 mpaka Januria 12 mwakani.

Tume imewataka walioteuliwa kugombea, mawakala na wananchi kwa ujumla kufuata sheria na taratibu za tume wakati wa kufanya kampeni.

Akizungumza jijini Kampala mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa tume hiyo, Simon Byabakama aliwataka wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia tahadhari ya kujikinga na visrusi vya corona.

“Wagombea wapo huru kuzindua ilani zao kabla ya kuanza kampeni. Tunataka kuwakumbusha kuwa kampeni zinafanyika huku kukiwa na tahadhari za ugonjwa wa covid -19 hivyo ni vyema kushirikiana katika kukinga wananchi na maambukizi ya virusi vya corona,” alisema.

Kati ya wagombea 11 wanaowania urais, yupo Rais wa sasa Yoweri Museveni aliyeshika madaraka kwa miaka 30 na mpinzani wake mkubwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi Ssentamu.

Wagombea wengine ni aliyewahi kuwa waziri wa ulinzi Henry Tumukunde, aliyewahi kuwa kamanda wa majeshi Mugisha Muntu, John Katumba na Nancy Linda Kalembe.

Chanzo: habarileo.co.tz