Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi mkuu Gabon: Rais Bongo atabiriwa ushindi

Uchaguzi Mkuu Gabon: Rais Bongo Atabiriwa Ushindi Uchaguzi mkuu Gabon: Rais Bongo atabiriwa ushindi

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: Voa

Serikali ya Gabon yenye utajiri wa mafuta imetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa rais, bunge na serikali za mitaa utafanyika tarehe 26 Agosti, wakati Rais Ali Bongo Ondimba akitarajiwa kushinda uchaguzi huo dhidi ya upinzani uliogawanyika.

Bongo bado hajatamka kama atagombea tena, lakini watu wengi wanamtarajia kugombea tena kiti chake.

Chama tawala Gabon Democratic Party (PDG) kinashikilia viti vingi katika mabaraza yote mawili ya bunge.

Rais Bongo mwenye umri wa miaka 64, aliirithi nafasi ya babake, Omar Bongo Ondimba, aliyeitawala nchi hiyo kwa muda wa miaka 41 hadi mwaka 2009.

Rais huyo alichaguliwa tena kwa kushinda kura chache sana mwaka 2016, ambapo alipata kura 5,500 tu zaidi ya mpinzani wake Jean Ping ambaye alidai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na wizi.

Bongo alipatwa na kiharusi mwaka 2018 na kukaa kando kwa miezi kadhaa wakati akijiuguza, na kuwaacha wapinzani wakihoji kama anafaa kuliongoza taifa hilo.

Familia ya Bongo imekuwa ikiitawala nchi hiyo kwa miaka 55 tayari imepewa chapa na upinzani kuwa ni sawa na utawala wa kifalme.

Lakini upinzani kwa mara nyingine tena umeshindwa kuafikiana kuhusu mgombea mmoja katika uchaguzi wa rais, na kusababisha wagombea takriban 15 kutangaza nia zao za kugombania kiti cha rais.

Chanzo: Voa