Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Liberia kuingia duru ya pili...

Liberia Uchaguzi Duru Uchaguzi Liberia kuingia duru ya pili...

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya muda ya uchaguzi wa rais nchini Liberia yanaonesha kuwa, Rais George Weah atachuana na mshindani wake wa karibu Joseph Nyuma Boakai kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo.

Matokeo ya asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa mpaka sasa yanaonesha kuwa, Weah ameshinda asilimia 43.8 ya kura, huku hasimu wake wa karibu, Boakai akiambulia asilimia 43.5. Mgombea anapasa kuzoa angalau asilimia 50 ya kura ili uchaguzi wa rais usiingie duru ya pili.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, Waliberia milioni 2.4 walikuwa wametimiza masharti ya kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia lililofanyika Jumanne ya Oktoba 10.

George Weah ambaye amewania muhula wa pili wa miaka 6 kupitia muungano tawala wa Coalition of Democratic Change (CDC) anasisitiza kuwa, kazi kubwa aliyowafanyia Waliberia hasa kuboresha sekta ya elimu na kuimarisha miundumsingi itamsaidia kushindi muhula wa pili.

Hata hivyo wakosoaji wake wanahisi kuwa hajafanya mengi ya muhimu tangu aingie madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2017.

Rais George Weah anatazamiwa kuchuana na Boakai katika duru ya pili ya uchaguzi huo, ikizingatiwa kuwa wagombea wengine 18 hawajapata zaidi ya asilimia 3 ya kura.

Ikumbukwe kuwa, Boakai aliyegombea akipeperusha bendera ya Chama cha Umoja alishindwa na George Weah katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live