Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Kiambaa: DP Ruto awarai wakazi kumchagua John Wanjiku

4afba387d81e29f6 Uchaguzi Kiambaa: DP Ruto awarai wakazi kumchagua John Wanjiku

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

William Ruto alimfanyia kampeni John Wanjiku ambaye anawania ubunge kupitia chama cha United Democratic Alliance (UDA)Nabu Rais aliwarai wenyeji wa Kiambaa kumchagua Wanjiku akisema ushindi wake utaashiria ushindi wa UDA mwaka ujaoUchaguzi huo umeandaliwa Jumanne, Julai 15 ambapo wenyeji watamchagua mbunge mpya baada ya kumpoteza kiongozi wao kutokana na COVID-19Naibu Rais William Ruto aliwasihi wenyeji wa Kiambaa kumpigia kura John Wanjiku katika uchaguzi mdogo wa Julai 15.

Akiongea nao kupitia kwa njia ya simu Jumatatu, Julai 12, Ruto aliwahimiza wakaazi kumpiga kura Wanjiku akisema kwamba ndiye kiongozi madhubuti kuwaongoza.

"Mnamo Julai 15 hebu tujitokezeni kwa wingi tumpigie kura Wanjiku. Yeye ni wa kazi ni kazi," alisema Ruto. Ninawaomba kwa unyenyekevu kumpigia kura," alisema.

Wakati uo huo, Ruto alitumia fursa hiyo kujipigia debe anapojiandaa kujitosa katika uwanja kuwania urais huku akiwarai wenyeji hao pia kumuunga mkono uchaguzi mkuu utakapofika.



Read also

Mtahiniwa wa KCSE Ajitoa Uhai Baada ya Kuandikia KNEC Barua

Wakazi wa Kiambaa watashiriki uchaguzi mdogo Alhamisi kumchagua mbunge mpya baada ya kiongozi wao Paul Koinange kuaga dunia.

Wanjiku ambaye ni mgombea wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) atamenyana na mpinzani wake mkuu Njama.

Kulingana na Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria matokeo ya uchaguzi huo yataashiria mambo yatakavyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kumuunga mkono Njama, kura hiyo imetajwa na wengi kuwa kivumbi kati yake na naibu wake William Ruto.

Viongozi hao wamekuwa wakitofautiana tangu 2018 huku rais akionekana kubadilisha mkondo kura ya 2022 inapokaribia licha ya kuapa kumuunga mkono naibu wake.

Baada ya Ruto kuhisi kuchezewa rafu alianza kampeni za mapema kujipigia debe kumrithi rais huku akiwaalika wageni nyumbani kwake Karen kuuza sera zake.



Read also

Mbunge Mpya wa Kabuchai Amjengea Nyumba Ajuza Aliyerauka Kumpigia Kura

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke