Mbunge wa Kenya ametoweka baada ya kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Magharibi mwa Kenya.
Walioshuhudia wanadai Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alimpiga mwanamume huyo kichwani wakati wa mabishano katika kituo cha kupigia kura kaunti ya Bungoma.
Polisi sasa wameanzisha msako wa kumtafuta mbunge anayewania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wamempa saa 24 kujisalimisha kwa mamlaka zinazochunguza mauaji hayo. Bw Barasa si mgeni katika mabishano.
Mwaka jana, alikamatwa na kushtakiwa kwa kumshambulia mwanamuziki wa nchini humo. Habari zaidi zinasema aliwahi kuhudumu katika jeshi.