Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi DRC 2023: Matokeo yatarajiwa hivi karibuni huku Rais Tshisekedi akiongoza

Uchaguzi DRC 2023: Matokeo Yatarajiwa Hivi Karibuni Huku Rais Tshisekedi Akiongoza Uchaguzi DRC 2023: Matokeo yatarajiwa hivi karibuni huku Rais Tshisekedi akiongoza

Sun, 31 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanatarajiwa hivi karibuni, huku Rais Félix Tshisekedi akifurahia kuongoza dhidi ya wagombea wa upinzani ambao wamedai uchaguzi urudiwe.

Rais Tshisekedi amepata takribani 72% ya kura hadi sasa, na anaonekana kujiandaa kwa muhula wa pili.

Uchaguzi wa Desemba 20 ulikumbwa na matatizo mengi ya vifaa. Ilibidi iongezwe hadi siku ya pili katika sehemu fulani za nchi.

Takribani theluthi mbili ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa, wakati asilimia 30 ya mashine za kupigia kura hazikufanya kazi, kwa mujibu wa waangalizi wa uchaguzi.

Mamilioni ya watu walisubiri kwa saa nyingi kabla ya kupiga kura, huku wengine wakikata tamaa na kurudi nyumbani.

Upinzani ulisema matatizo hayo ni sehemu ya mpango wa makusudi wa kuruhusu matokeo kuchakachuliwa ili kumpendelea Bw Tshisekedi.

Mkuu wa tume ya uchaguzi hapo awali alisema wagombea wa upinzani wanataka uchaguzi mpya kwa sababu "wanajua walishindwa... ni walishindwa vibaya". Mkuu wa uchaguzi Denis Kadima alikiri kuwepo kwa dosari kadhaa lakini akasisitiza kuwa matokeo yaliyotangazwa hadi sasa yanaakisi matakwa ya watu wa Congo. Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, tayari amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa X akimpongeza Bw Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live