Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi DR Congo: Shughuli ya upigaji kura yacheleweshwa kwa muda mrefu

Uchaguzi DR Congo: Shughuli Ya Upigaji Kura Yacheleweshwa Kwa Muda Mrefu Uchaguzi DR Congo: Shughuli ya upigaji kura yacheleweshwa kwa muda mrefu

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Shughuli ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekumbwa na ucheleweshaji wa muda mrefu katika vituo vya kupigia kura.

Wapiga kura walisubiri kwenye foleni ndefu katika vituo vingi vya kupigia kura katika mji mkuu, Kinshasa, na miji mingine kwani walichelewa kufunguliwa vituo kwa takriban saa mbili.

Karatasi za kupigia kura ziliwasilishwa dakika za mwisho katika uchaguzi ambao umeonekana kuwa na tatizo la ukosefu wa vifaa.

Rais FĂ©lix Tshisekedi anachuana na wagombea 18.

DR Congo ni takriban mara nne ya ukubwa wa Ufaransa, lakini haina miundombinu ya kimsingi - hata baadhi ya miji yake kuu haijaunganishwa na barabara.

Umoja wa Mataifa, Misri na nchi jirani ya Kongo-Brazzaville zilisaidia kusafirisha nyenzo za uchaguzi katika maeneo ya mbali.

Takriban watu milioni 44 wamejiandikisha kupiga kura, kufuatia kampeni iliyotawaliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Katika mji wa kaskazini-mashariki wa Bunia, watu ambao hapo awali walikimbia ghasia na hawakuweza kusafiri kurejea vijijini kwao kupiga kura walionyesha hasira yao kwa kushambulia kituo cha kupigia kura na kuharibu mashine za kupigia kura kabla ya polisi kurejesha utulivu.

Chanzo: Bbc